Kampuni ya Ufaransa yakana dai

Taifa Leo - - NEWS - Na AFP

KAMPUNI ya Ufaransa inayosimamia mitambo ya kieletroniki ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), imekanusha madai kuwa mitambo hiyo ilidukuliwa.

Ot-morpho, ikijibu madai ya muungano wa upinzani, NASA, ilisema “uchunguzi wa kina” wa mitambo hiyo, almaarufu, KIEMS, unaonyesha kuwa madai ya NASA ni uongo.

Kwenye barua kwa serikali ya Ufaransa, mgombeaji urais wa NASA Raila Odinga anaikashifu Ot-morpho kwa kuruhusu kudukuliwa mitambo yake na kuhifadhi data kuhusu uchaguzi, na ile ya kutuma matokeo, bila idhini.

Bw Odinga (pichani kushoto) alisema kuingiliwa kwa mitambo hiyo ndiko kulipelekea kubadilishwa na hesabu za kura za urais.

Lakini Afisa wa mkuu wa Ot-morpho, Frederic Beylier aliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kwamba ukaguzi uliofanywa kwa usaidizi na kampuni kadha, ulionyesha kuwa mitambo hiyo kwamba “haikuingiliwa kupitia uvurugaji wa data, udukuzi, wala kufunguliwa kwa njia yoyote bila idhini maalum.”

Kampuni hiyo iliuzia Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) mitambo 45,000 ya KIEMS iliyotumiwa kuwatambua wapigakura kieletroniki na zile zilitumiwa kutuma matokeo baada ya kuhesabiwa vituoni.

Mitambo hiyo pia ilitumiwa kutuma picha za fomu za 34A na 34B zilizotumiwa kujumuisha kura

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.