Tume yalia dhuluma za kike kuongezeka

Taifa Leo - - NEWS - Na Carolyne Agosa

TUME ya Kitaifa ya Jinsia na Usawa, imeelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la matamshi na visa vya dhuluma za kijinsia dhidi ya wanawake.

Tume hiyo inataka wahusika kukamatwa mara moja na polisi kuwafungulia mashtaka ya uhalifu.

NGEC ilishutumu vikali kizaazaa kilichotokea katika hoteli ya Jumuia mjini Kisumu kundi la vijana lilipovamia mkutano wa viongozi wanawake wa amani.

Vijana hao walizua fujo wakidai kikao hicho kilikuwa kikitumika kununua vitambulisho vya wakazi ili kuiba kura katika marudio ya uchaguzi wa urais Oktoba 17.

“Tulishuhudia kisa cha kutamausha wanawake wakidhulumiwa na kuibiwa wazi wazi mchana na vijana wahuni.

“Kando na kwamba shambulizi hilo halikuwa na msingi wowote, ni makosa kwa vijana hao kuchukua sheria mikononi mwao kuwahangaisha wanawake,” akasema mwenyekiti wa NGEC Bi Winfred Lichuma.

Aliongeza: “Tunamtaka Inspekta Jenerali wa Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma kuwakamata wahusika hao mara moja na kuwafungulia mashtaka ya uhalifu.”

Bi Lichuma aliambia Taifa Jumapili kuwa, iwapo itathibitishwa mbunge alitoa matamshi hayo anafaa kuchukuliwa hatua kali.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.