Mandago ataka Wizara ya Fedha itoe pesa haraka kuendesha kaunti

Taifa Leo - - NEWS - Na Titus Ominde

GAVANA wa Uasin Gishu Jackson Mandago ametaka wizara ya Fedha kutoa pesa kuendesha shughuli katika kaunti.

Bw Mandago alisema utawala wake uko tayari kuendelea kuhudumia wananchi mashinani, na kwa hivyo wizara husika yapaswa kutoa fedha ambazo zimetengewa kaunti kuendeleza miradi yake.

Akihutubu mjini Eldoret, Bw Mandago alisema mvutano wa kisiasa ulioko kati ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa Nasa Raila Odinga kuhusiana na kurudiwa kwa uchaguzi wa urais, haupaswi kuathiri shughuli za maendeleo ya kaunti.

“Sisi kama kaunti tuko tayari kuendelea kuhudumia wananchi tunataka waziri wa fedha Bw Henry Rotich kutupa fedha za kuendeleza shughuli za kaunti,” alisema Bw Mandago.

Alisema atatumia awamu yake ya pili kukamilisha miradi ambayo aliianzisha kwenye kipindi cha kwanza cha uongozi wake. Kwa hivyo aliwataka wakazi wasitarajie miradi mipya.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.