Bi Kenyatta arai wakazi wajitokeze kwa wingi wampigie kura mumewe

Taifa Leo - - NEWS - Na Oscar Kakai

MKEWE Rais Bi Margaret Kenyatta alimpigia debe mumewe katika kaunti ya Pokot Magharibi, na kuwarai wakazi kutoka kaunti saba za eneo la Kaskazini mwa Ril Valley kujitokeza kwa wingi na kumpa ushindi Rais kwenye marudio ya uchaguzi.

Akiongea jana katika uwanja wa maonyesho ya kilimo ya Kishaunet mjini Kapenguria, Bi Kenyatta alisema kuwa Rais Uhuru Kenyatta astahili kupewa awamu ya pili kuongoza nchi.

“Ninawaomba nyote mjitokeze kwa wingi tarehe kumi na saba Oktoba. Lazima tuhakikishe chaguo letu ni Uhuru Kenyatta kama Rais. Ili kupata ushindi, twahitaji ushirikiano na kutafuta kura zote ambazo hatukupata,” akasema.

Bi Kenyatta aliwahakikishia akina mama kuwa Rais Kenyatta huchukulia shida za wanawake kwa uzito na kuhakikisha kuwa wasiojiweza wanafaidika.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.