Ujumbe Mfupi

Taifa Leo - - BARUA -

MAONI: MTAFARUKU umeibuka miongoni mwa wachungaji wa kanisa la Pentecostal Assemblies of God (PAG) siku moja tu baada ya Naibu Rais William Ruto kuhutubia kongamano lao Vihiga. Je, unakubaliana na wachungaji hao kwamba viongozi wengi wa kidini wamegeuza mikutano ya maombi kuwa jukwaa la wanasiasa kusaka kura?

Ni kweli. Tena hiyo cheki ya Sh10 milioni ni ng’o. Waliuziwa mbuzi kwenye gunia, wao sio wa kwanza kuahidiwa. Masero, Kuria

Hapo ni kweli. Unapoalika mwanasiasa kanisa umealika siasa. Lazima mwanasiasa anapohutubu aongee siasa. Kibise, Sabasaba

Ni wazi viongozi wengi wa makanisa wamepotoka maadili kwa kuegemea siasa. Wamesahau jukumu lao la kuongoza kanisa ikiwemo wanasiasa. Hata hivyo, si vibaya wanasiasa kusaka kura kanisani kwani waumini pia ni wapigakura. Nashauri wanasiasa waandike hotuba watatoa kanisani ili wasipotoke na kuropoka.

Imbiakha, Idakho

Siku hizi kanisa zimekuwa himaya za wanasiasa kuacha donge nono. Mbona wachungaji hawawakemei wakiwepo. Cege Kariuki

Mambo ya kanisa hayaambatani na siasa.

Omena wa Moi’s Bridge

Wachungaji wako sawa kabisa. Ernest, Mumias

Ndio. Wakati huu wa kampeni makanisa mengi yamenaswa na mtego wa wanasiasa kwa ajili ya pesa. Hawa wanasiasa hawaendi tu kanisani kwa sababu ya maombi.

Plumber Muchiri, Karumandi

MJADALA WA LEO: GAVANA wa Nairobi Mike Sonko, amejipata taabani baada ya kutangaza kuwa magari ya uchukuzi wa umma (PSVS), hayataingia katikati mwa jiji kuanzia Jumatano. Shirikisho la Kutetea Wateja (Cofek) linataka gavana aunde kwanza mfumo mwafaka na nafuu wa kuvusha watu upande wa pili, vituo vya magari ya moshi na steji kadha za mabasi. Je, marufuku hiyo itekelezwe ama mfumo kabambe wa utekelezaji uundwe kwanza?

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.