Ni makosa makubwa kukosoa Maraga hata kabla uamuzi wa kina kutolewa

Taifa Leo - - BARUA -

MIITO ya kumtimua Jaji Mkuu na rais wa Mahakama ya Juu David Maraga na lawama chungu nzima hazina msingi wowote.

Ukweli uliopo ni kwamba Jaji Maraga pamoja na majaji wengine sita wa mahakama hiyo kuu zaidi nchini hawakukosea chochote katika kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa Rais Uhuru Kenyatta.

Wale wanaomkosoa Jaji Maraga hata kabla ya kusomwa kwa uamuzi wa kina kuhusu ufisadi uliokithiri wakati wa zoezi la uchaguzi mkuu wa Agosti 8, 2017 wanakosea.

Kile ningeliwashauri ni kuwa na subira ndipo wajue maelezo kamili ya kubatilisha uchaguzi huo.

Kile kingine nataka kuwakumbusha waliojitosa katika lindi la kumtupia cheche za maneno Jaji Maraga ni kwamba kila jaji huamua kesi kulingana na ushahidi uliowasilishwa na sheria iliyopo. WAKILI ALFRED NYANDIEKA Nairobi

Muthama hakuwa na makosa

WADADISI wengi wa masuala ya kisheria wamekosoa kesi aliyoshtakiwa aliyekuwa Seneta wa Machakobs Johnson Muthama kuwa haina mashiko kiheria kwa matamshi anayodaiwa alisema ya uchochezi ni mchongoano tu.

Shtaka hili liliposomwa wahakiki wa masuala ya sheria kortini waliangua kicheko na kuuliza ikiwa kiongozi wa mashtaka ya umma amesahau sheria.

Kile Muthama alidaiwa alisema cha kuchochea ghasia ni kumtaka Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wakutane naye Muthama na mwanasheria shupavu James Orengo wote wakiwa wamevaa glovu wachapane makonde ndipo kiongozi wa nchi ajue kilichomtoa kanga manyoya.

WAFULA JUMA

Kakamega

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.