Demu akana sponsa wake akidai kuwa alimpotezea wakati bure

Taifa Leo - - DONDOO! - Na John Musyoki

DEMU mmoja kutoka sehemu hii, alikana sponsa wake mbele ya watu akidai buda alikuwa akimpotezea wakati.

Duru zinasema demu alikuwa katika uhusiano na buda huyo kwa muda mrefu lakini akaamua kumtema baada ya kutambua kuwa alikuwa akimpotosha.

Siku ya kioja buda alikutana na demu huyo mtaani akiwa na wenzake na akamuita chemba wazungumze lakini demu alimpuuza na kuanza kumrushia maneno ya kumuudhi.

“Hi Darling, kuja tuzungumze kidogo halafu uendelee na safari yako. Hata ukipenda nitakupa lili wakati utakapokuwa ukirudi nyumbani,” buda alimuomba demu.

Kinyume na matarajio ya buda huyo, demu alianza kumfokea na kumlaumu. “Tafadhali sina muda wako.sitaki maneno yako. Kwa muda nimefuata tabia zako nikajua ni za uogo na za kupotosha. Jipe shughuli na usaidizi wako sitaki. Nikome kabisa na usiwahi kuniita darling, ushasikia.nenda ukatafute mjinga wa kudanganya,” demu aliwaka.

Sponsa hakuwa na la kufanya ila kuchomoka kabla ya kuaibishwa zaidi mbele ya watu na kuacha kipusa akipiga gumzo na wenzake.

Haikujulikana kilichojiri baada ya kioja hicho.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.