Amlilia mkwewe kuhusu ulevi, kutojali kwa mkewe

Taifa Leo - - DONDOO! - Na Dennis Sinyo

JOMBI wa hapa, alizua kioja baada ya kumlilia mama-mkwe akidai mkewe alikuwa amesahau majukumu yake na kugeukia ulevi wa kupindukia.

Jamaa alisema alilazimika kuacha kazi baada ya watoto wake kuanza kutaabika kwa kukosa mtu wa kuwatunza na hata kuwapikia.

“Mimi sina amani hata kidogo na ilibidi niache kazi ili kuwalea watoto kwa sababu wanaumia sana huku mama yao akilewa ovyoovyo,” alisema jamaa huyo.

Duru zaarifu mke wa jamaa alikuwa amegeukia ulevi wa kupindukia na kusahau kwamba alikuwa na watoto.

Alikuwa akilewa chakari hadi kufikia kiwango cha kushindwa kutembea na kuanguka njiani. Jamaa aliamua kwenda kumlilia mama mkwe kwamba alikuwa amechoshwa na tabia ya mkewe. Hata hivyo, inasemekana mama mkwe alijiondolea lawama na kusema hangemsaidia jamaa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.