Ajabu mlevi kuwashauri kina mama kulea watoto

Taifa Leo - - DONDOO! - Na Richard Maosi

MLEVI wa eneo hili, aliwashtua wapangaji katika ploti anamoishi, alipoanza kuwashauri akina mama jinsi ya kulea watoto wao.

Jamaa alipayuka akiwashtumu wanawake kwa kutumia wakati wao mwingi kupiga udaku na kuwaacha wanao kucheza barabarani bila mtu wa kuwaangalia.

“Kwanza wewe mama, watoto wako ni wanyonge sana, kwani hawashibi siku hizi? Ama unawanyima chakula?”alianza kwa kumfokea mama mmoja aliyejaribu kumwonyesha kiburi.

Ilibidi wenzake kukunja mkia na kutazama chini kwa aibu kwani kila aliyejaribu kubishana naye, alinyamazishwa kwa matusi.

Kuanzia siku hiyo wanawake hao walichukua tahadhari kubwa kila wanapomuona jamaa akitoka kukata maji huku wakazi wakisema aliwarudisha akina mama hao wanaofahamika kwa umbea.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.