Polo aaibisha boma kwa kutegemea jasho la mke

Taifa Leo - - DONDOO! - Na Nicholas Cheruiyot

MLOFA wa hapa, alisutwa na ndugu zake kwa kuaibisha boma kwa kumtegemea mkewe kwa kila kitu.

Mdaku alisema kwamba polo huwa ameng’ara kila siku na kushinda akiwafuata wanasiasa na baadaye kurudi nyumbani akiwa mikono mitupu.

“Kila mtu huwa akimhurumia shemeji kwa kuumia kufanya vibarua huku ukivaa suti na kurandaranda tu. Huoni aibu ukila cha mkeo? Mwanamume ni kukimu familia bwana,” jamaa alisutwa na ndugu zake.

Yasemekana mlofa alijitetea kuwa, anasaka kazi ya ofisi itakayompa donge nono lakini ndugu zake wakamwambia aanze kutafuta kazi za mikono huku akiendelea kusaka ajira anayotamani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.