Namna Maraga alivyohakikisha ushawishi wa nje unazimwa

Taifa Leo - - JAMVI - Na WYCLIFFE MUIA

MKESHA wa kuamkia Ijumaa ya kutangazwa kwa uamuzi wa Mahakama ya Juu uliofutilia mbali matokeo ya kura za urais, ulisheheni njama kali za kisiasa zilizolenga kushawishi misimamo ya majaji kuhusiana na uamuzi wa kesi hiyo.

Majaji wanne kati ya majaji sita waliosikiza kesi hiyo walikubaliana na kinara wa muungano wa NASA Raila Odinga kuwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Agosti nane haukuandaliwa kulingana na sheria.

Katika uamuzi huo wa kihistoria uliotikisa dunia nzima, majaji Jackton Ojwang’ na Njoki Ndung’u walipinga uamuzi wa kufutilia mbali ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta.

Jaji Mkuu David Maraga, naibu wake Philomena Mwilu, Jaji Smokin Wanjala na Jaji Isaac Lenaola waliridhika na ushahidi uliowasilishwa na upinzani na kuamua kwa kauli moja kutupilia mbali ushindi wa Rais Kenyatta na kuagiza uchaguzi mwingine wa urais uandaliwe katika kipindi cha siku 60.

Hata hivyo, uamuzi huo uliafikiwa kukiwa na shinikizo nyingi za kisiasa zilizopelekea Bw Maraga aagize majaji wote wazime simu zao ili kujadiliana bila presha kutoka nje.

Baada ya mawakili wa pande zote kumaliza kuwasilisha hoja zao mbele ya mahakama, majaji wote sita walikongamana katika hoteli moja mtaani Upper Hill, Nairobi.

Muda mfupi baadaye majaji hao walihamia sehemu nyingine faraghani na kukubaliana wazime simu zao za mkononi. Hata hivyo, hatua hiyo haikuzuia maajenti wa kisiasa kuwafikia.

Mmoja wa majaji anashukiwa kudokezea chama cha Jubilee kuwa huenda uamuzi wa mahakama ukamfaa Bw Odinga, hatua ambayo ilizua wasiwasi mkubwa serikalini.

Hatua hii ilipelekea Ikulu kuandaa kikao cha dharura kilichopanga njama ya kushawishi angalau jaji mmoja au zaidi kubadili msimamo ili kumpa Rais Kenyatta ushindi katika kesi hiyo.

Duru zinasema waziri mmoja akiandamana na mawakili wawili walitembelea mmoja wa majaji nyumbani kwake kumfahamisha kile walichotaja kama ‘msimamo wa serikali’ kuhusu kesi hiyo

Duru zinasema jaji huyo aliwakaribisha na kuwafahamisha kuwa uamuzi wa mwisho wa mahakama utazingatia sheria na ustawi wa taifa.

Ujumbe wa Jubilee ulishawishika kuwa maelezo ya jaji huyo yaliashiria kuwa uamuzi wa majaji utawafaa na hata wakili husika akatumia vinara wakuu wa Jubilee habari kuwa ‘wameshinda kesi’ KUTOKA Uk 13

Picha/dennis Onsongo

Jaji Mkuu David Maraga na mkewe Yucabeth Nyaboke wakihudhuria ibada katika kanisa la Seventh Day Adventist, Nairobi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.