Buhari kutua London ziarani alikotibiwa

Taifa Leo - - HABARI ZA AFRIKA NA DUNIA -

RAIS wa Nigeria Muhammadu Buhari atatua kwa muda jijini London, ambako aliishi kwa miezi mitano mwaka huu akitibiwa, akiwa njiani kutoka Amerika baada ya kuhudhuria Kongamano la Viongozi wa Mataifa Wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN), msemaji wake amesema.

Buhari ataondoka Nigeria leo kueleka makao makuu ya UN jijini New York, kulingana ujumbe wa barua pepe uliotumw na msemaji wake, Femi Adesina.

Hii ndio itakuwa mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kufanya safari ya nje ya Nigeria tangu aliporejea nchini humo kutoka Uingereza mnamo Agosti 19. Alikuwa akipokea matibabu baada ya kuugua ugonjwa ambao haukufichuliwa. Akiwa Amerika, Buhari atakutana na Rais wa Amerika Donald Trump na viongozi wengine, akasema Adesina. Lakini akaongeza. “Rais Buhari pia atatua kwa muda jijini London akiwa njia akirejea nchini

Msemaji huyo hakufafanua ikiwa Buhari anapokea matibabu jijini London au la, kwani alidinda kutoa maelezo zaidi kuhusu suala hilo.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.