Serikali kuwajengea wakimbizi makazi wasiishi mahemani

Taifa Leo - - HABARI ZA AFRIKA NA DUNIA -

SERIKALI ya Bangladesh itawajengea maelfu ya wakimbizi wanaofurika nchini humo makazi 14,000.

Wakimbizi hao kutoka kabila la Rohingya, na ambao ni Waislamu, wamekuwa wakiishi ndani ya mahema kando ya barabara, milimani na kwenye viwanja, maafisa walisema jana.

Kulingana na takwimu kutoka Umoja wa Mataifa (UN) takriban wakimbizi 400,000 wa asili ya Rohingya wamekuwa wakiwasili Bangladesha tangu Agosti 25 kukwepa operesheni za wanajeshi wa Myanmar wanaojibu mashambulio ambaye yamekuwa yakifanywa na waasi wa Rohingya.

Watawala wa Bangladesh wanasema watajenga kambi kubwa katika ardhi yenye ukubwa wa ekari 2,000 karibu na kambi ya wakimbizi wa Rohingya mjini Kutupalingo, Wilayani Cox Bazar. Wilaya hiyo inapakana na jimbo la Myanmar.

“Serikali iliamua kujenga makazi 14,000 ambako wakimbizi 400,000 wa Rohingya wataishi.” Katibu msimamizi wa shirika la kushughulikia majanga Bangladesha Shah Kamal aliambia shirika la habari la AFP.

“Tumetakiwa kujenga nyumba hizo ndani ya muda wa siku 10. Kila nyumba inahifadhi familia sita,” akasema akiongeza kuwa kambi hiyo ina maji na vyoo na vituo vya kutoa huduma za matibabu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.