Mvua yaua 54, hasara tele

Taifa Leo - - HABARI ZA AFRIKA NA DUNIA - Na AFP

WATU 54 walikufa huku wengine 200,000 wakiachwa bila makao yao kutokana na athari za mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyoshuhudiwa nchini Niger, Umoja wa Mataifa (UN) umesema.

Shirika la UN kuhusu Misaada ya Kibinadamu (OCHA) lilisema vifo vingi vilitokea katika jiji kuu la Niamey ambapo zaidi ya makazi 11,000 yaliharibiwa.

Miji mingi iliyoathirika katika mkasa huo ni Dosso, iliyoko kusini mwa nchi hiyo, Tillaberi (Magharibi), Maradi na Zinder.

Mwaka jana watu 50 walifariki katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Maafisa wa serikali walisema mkasa huo utaathiri shughuli za uzalishaji chakula kwani ekeri 12,000 za mashamba ziliathiriwa, UN ilisema.

Vile vile, zaidi ya mifugo 16,000 iliangamizw na mafuriko hayo.

Thuluthi tatu ya ardhi ya taifa hilo lenye watu milioni 17 ni jangwa.

Nchi hiyo hukumbwa na njaa kutokana na kiangazi cha kila mwaka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.