Mugabe ampa mkewe nafasi kuu chamani

Taifa Leo - - HABARI ZA AFRIKA NA DUNIA -

RAIS wa Zimbabwe Robert Mugabe amemteua mkewe, Grace, katika wadhifa mkuu ndani ya chama tawala, Zanu- PF katika hatua ambayo wakosoaji wake wanasema ni njama ya kumweka katika nafasi bora kufanikisha ushindi wa rais huyo uchaguzini.

Mugabe amemteua mkewe kuwa mwanachama wa kamati kuu itakayosimamia uchaguzi mkuu wa mwaka ujao 2018 .

Kamati hiyo yenye wanachama watano itaongozwa na Waziri wa Serikali za Mitaa Savior Kasukuwere.

Wanachama wengine watakuwa Waziri wa Fedha Patrick Chinamasa, Ignatius Chombo (Masuala ya Ndani) na Katibu wa kundi la Vijana wa Zanu-pf Kudzanai Chipanga.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.