Kukinai

Taifa Leo - - SOKOMOKO -

Nalekeza kwa Jalali, mikono nikiamini, Mola asotenda feli, ndiye wa kutuauni, Bwana Mola takabali, dua na tupe imani, Kukinai ikhiwani, kwetu kunayo thamani.

Wizi na ubaradhuli, tutendao insani,

Na yote ya kikatili, kuna jambo yabaini, Tungafunga na kusali, bado tuna kubwa deni, Kukinai ikhiwani, kwetu kunayo thamani.

Mfano ni maakuli, tulapo kwenye sahani, Ama ni kwenye bakuli, lililojazwa pomoni, Ni tule kwa taamuli, shibe imo humo ndani, Kukinai ikhiwani, kwetu kunayo thamani.

Pesa zinazo shughuli, kwetu sote duniani, Na tunazo sampuli, za kuzisaka wendani, Ila zile za halali, kwetu ni bora jamani, Kukinai ikhiwani, kwetu kunayo thamani. MOHAMMED SHABAN ALI ‘Mpembuzi Mchanga’ Mbungoni, Mombasa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.