Ngoma ngomani

Taifa Leo - - SOKOMOKO -

Nafunga zangu kibwaya, ngomani najitundika, Na kwa kujimwayamwaya, huku nikihadaika, Watu wasio na haya, kati wanaburudika, Napiga ngoma ngomani, mwenzenu naburudika.

Kweli kataka mwenyewe, kwa barua kuandika, Sikurusha langu jiwe, hata ulimbo kuweka, Kuku kanasa mwenyewe, kitanzi kajitundika, Napiga ngoma ngomani, mwenzenu naburudika.

Sikuremba kumchinja, kwani angeporochoka. Mngeniona kanjanja, nisiyesakata soka, Kumbe fundi wa bakunja, na viduku kuviruka, Napiga ngoma ngomani, mwenzenu naburudika.

Kilichobaki mahari, kwao nishatambulika, Hakika fundi mahiri, mamba nimekamatika, Mawanda yamekithiri, mwenzenu nagarauka, Napiga ngoma ngomani, mwenzenu naburudika. MFAUME HAMISI ‘Fimbo ya Kale’

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.