Hasira hasara

Taifa Leo - - SOKOMOKO -

Hasira zina hasara, zijapo ni kupagawa, Hasira bila subira, hakuna la kujaliwa, Hasira kwa maghufira, na subira ndio dawa, Hasira kweli hasara, tangu Adamu na Hawa.

Hasira kila hasara, zimekwisha hukumiwa, Hasira mwenye dhamira, akumbuke ya pakawa,

Hasira siyo nusura, bighairi ya beluwa, Hasira yake ngonjera, mwisho ni kulaaniwa.

Hasira yake madhara, na wazimu ni fahuwa, Hasira siyo busara, ni kakara kuzuzuwa, Hasira hazina sera, za zogo kutatuliwa, Hasira yake majira, kujiri ni kulemewa.

Hasira huteka nyara, akili zikichachawa Hasira hazina dira, yakajiri maridhawa, Hasira mtu hugura, peke aishi ukiwa, Hasira si masihara, ni majuto kujiliwa.

Hasira yake jahara, sauti ingapaziwa,

Hasira kukosa kura, ya kila mtahiniwa,

Hasira hazina sera, ya wema kushindaniwa, Hasira ipi bishara, ya faraja kungojewa? ABDALLAH MASKINI ‘Cha Mtema Kuni’ California, Taveta

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.