Nirudiye mpenzi

Taifa Leo - - SOKOMOKO -

Haki nandika baruwa, huku miye nalia, Kinilizacho ukiwa, mpenzi kunikimbia, Haji kuniokowa, kwenye penzi nangamia, Nirudiye we mpenzi, Andende nakuhitaji.

Huku niliko mpenzi, sina la kukuambia, Kakika yako majonzi, mno yamenivamia, Ni kilio na simanzi, miye uloniachia, Nirudiye we mpenzi, Andende nakuhitaji.

Ingekuwa bora sana, tena ningeshangilia, Mpenzi wewe kuonana, japo kwa ubahalia, Baridi tungetoana, na makiwa ya dunia, Nirudiye we mpenzi, Andende nakuhitaji.

Hakika mawazo yako, taharuki hunitia, Sikihaha mwenzi wako, mpenzi kukufikiria, Sijui huko uliko, kwenye penzi naumia,

Nirudiye we mpenzi, Andende nakuhitaji. THOMAS KOCHWA ‘Malenga wa Kismati’ Nairobi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.