Tumezinduka

Taifa Leo - - SOKOMOKO -

Maono yenu si yetu, hilo tumeling’amua, Medani zenu si zetu, bado hilo twagundua, Mkiwasha moto katu, si wetu twawaambia, Manake tumezinduka, hila zenu twang’amua.

Mwaanzisha nyingi vita, kinaya hampigani, Mwatuacha twafa vita, kijificha kasrini, Kwetu hali kizorota, mwacheka majifichoni, Mwajitoa kukipoa, kilia yale ya mamba.

Ona mwauwasha moto, huku mwaogopa joto, Twaitika wenu mwito, zitimie zenu ndoto,

Ila mkipata pato, mwatuona viroboto, Mwadhani sisi ni nduli, kisahau letu penzi.

Bila soni ndugu ona, undugu mwauharibu. Si wetu wale nanena, japo kwenu ni sahibu, Kwa panga shoka twapigana, kwa sababu yenu babu,

Ila sasa mezinduka, hila zenu hatushiki. MWANGANGI IKUNGA

Baraton TTC

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.