Wapi zitatupeleka?

Taifa Leo - - SOKOMOKO -

Wakubwa msiudhike, leo ninaulizia, Wala msibabaike, nchi yetu natetea, Na siasa zifanyike, taratibu nawulizia, Siasa za upinzani, wapi zitatupeleka?

Tunapozidi kampeni, na matusi tuachie, Na vitisho tuacheni, siasa duni tuwachie, Muendapo ziarani, amani mzingatie, Siasa za upinzani, wapi tutazipeleka?

Vijana jihadharini, tusije tukachochea,

Ukosefu wa amani, na watu kuteketea, Matokeo kubalini, tuishi kifamilia,

Siasa za upinzani, wapi zitatupeleka? ALEXANDER MUTETHIA Kithangaini, Machakos

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.