Nimenawa mikono

Taifa Leo - - SOKOMOKO -

Ukiona mekuchoka, niondokea machoni, Usinitie mashaka, ikatoweka amani,

Wala sitokurupuka, nikakujia mwandani, Meosha mikono kwako, sina haja nawe tena.

Ulichonacho kiburi, mithili yako hakuna, Huluka yako kaburi, huishiwa la kunena, Huezi kutasiwiri, mbali tulikokumbana, Meosha mikono kwako, sina haja nawe tena.

Ufurishe lako shavu, picha gani waonyesha, Umekua kama kovu, kweli umeshanichosha, Narejea kwetu Jomvu, nikaghairi maisha, Meosha mikono kwako, sina haja nawe tena. ABBAS MOHAMMED

‘Malenga Mzito’

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.