Equity, USIU katika gozi la marudiano

Taifa Leo - - SPOTI - Na Caxton Apollo

KLABU ya Equity Bank itakutana na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha USIU-A katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu ya Mpira wa Vikapu ya Wanawake uwanjani Nyayo leo. Equity, ambayo inatetea taji, ilibwaga USIU-A Flames kwa alama 65-32 katika mechi ya mkondo wa kwanza. Washambuliaji matata wa Equity, Hilda Indasi, Mercy Wanyama na Susan Akinyi bado wana makali ya kuwawezesha kuandikisha ushindi mwingine.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.