Ngoliba yalimwa na Magogoni FC

Taifa Leo - - SPOTI - Na Lawrence Ongaro

NGOLIBA FC ililimwa 2-1 na Magogoni FC katika mechi safi ya kirafiki katika Shule ya Msingi ya Gatuanyaga, juzi. Vijana wa Magogoni walipata bao la ufunguzi kutoka kwa James Maina dakika ya 20. John Mwangi alisawazisha 1-1 dakika ya 32 kabla ya mshambuliaji matata George Kimani kufunga bao la ushindi dakika ya 65. Kwingineko, Clepton ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Muguga Stars.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.