Usibishe, bado yule yule

Taifa Leo - - FRONT PAGE -

BAADA ya mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino kukamatwa tena muda mfupi tu baada ya kuachiliwa kwa dhamana, Alhamisi kuliibuka posti kwenye akaunti yake ikisema mbunge huyo hajulikani aliko kufuatia yeye kuhamishwa kutoka kituo cha polisi cha Pangani na kupelekwa kusikojulikana. Babu amekuwa akitrendi sana juma lote hili toka atupwe ndani kwa madai ya kumtusi Rais.

Dominic Murunga: Wakati umefika sasa kwa wengine wetu kujitenga tuwaachie Wakalenjin na Wakikuyu nchi yao.

Rita Njiru: Sijui kwa nini watu wengine wana catch mafeelings wakati hata Rais mwenyewe aliwatusi majaji. Badala ya kuposti huu upuzi wakati huna lolote mbona usiiombee taifa huu ukabila tulionao ukwishe.

Benmidigo Odhiambo: Babu kila kitu kitakuwa sawa. Naona Raila Odinga wa pili akiamka, kama sio wewe na Raila Amollo ni kina nani wataikosoa hii serikali? Nakuombea mema.

Alphaxard Makori: Badala ya hawa polisi kutumia nguvu nyingi kupita maelezo kumkamata Babu, mbona wasizielekeze kuwasaka wauaji wa Jacob Juma na Chris Msando.

Adon Jakinda: Hawa vibaraka wa Jubilee wanasahau kuwa Kenya ni taifa lenye Demokrasia. Muueni Babu Owino na mvuruge amani Kenya.

Ton Rajde: Taratibu Kenya inarudi katika zile enzi za Nyayoism. Haina tofauti sana na enzi za Adolf Hitler na Iddi Amin ila hawakuishi milele.

Sarah Gathoni: Lakini si nadhani aliachiliwa baada ya kutoa pesa. Au amepelekwa Kapenguria?

Linda: Watu walioababisha post election vilolence wako huru, wale waliotuibia Euro Bond na pesa za NYS wako huru, hata Waiganjo hakudhalilishwa kihivi.

Jianah Wanga: Blunder Jubilee wanaeza fanya ni kuumua Babu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.