Raila akemea serikali kuzuia Kalonzo, Weta kusafiri

Taifa Leo - - FRONT PAGE - Na BERNARDINE MUTANU

Kinara wa NASA Raila Odinga ameikemea Serikali kwa kuwazuia vinara wenza Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula kusafiri nje ya nchi.

Vinara hao walikuwa wakielekea Uganda kwa hafla ya kuhitimu kwa wanafunzi wa chuo kikuu.

Jana, Bw Musyoka ambaye ni mgombea mwenza wa Bw Odinga kwenye Uchaguzi wa Urais unaopangwa kurudiwa Oktoba 27, alikuwa ameamndamana na Bw Wetang’ula walipozuiwa katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Kwa mujibu wa Bw Odinga, wawili hao walitakiwa na maafisa wa usalama kwenye uwanja huo, waonyeshe barua ya kuwaruhusu kutoka Ikulu.

ya kuwaruhusu kutoka Ikulu.

Bw Musyoka ndiye chansela wa Chuo Kikuu cha Teknolojia na Usimamizi cha Uganda na alipaswa kuongoza hafla ya kufuzu leo.

Akiwa na Bw Wetang’ula, vinara hao wa NASA walizuiliwa kwa zaidi ya saa nzima kabla ya kuachiliwa.

Jana akihutubia wanahabari katika makao makuu ya Okoa Kenya, Lavington, Nairobi Bw Odinga alishutumu serikali kwa hatua hiyo aliyosema ni ukiukaji wa sheria.

Kinara huyo alisema hali ya kisiasa inazidi kudhoofika nchini kwa kuelezea kuwa viongozi hao walifahamishwa na polisi kuwa walifaa kupata idhini kutoka Ikulu ili kutoka nje ya nchi.

“Majaribio ya kuwazuia viongozi wa upinzani kuondoka nchini na kufuatilia wanakoenda kwa kuwataka kupata idhini kutoka Ikulu ni ukiukaji wa sheria na serikali,” alisema kiongozi huyo wa ODM.

“NASA inashutumu ukiukaji wa haki na uhuru na dhuluma dhidi ya uongozi wake,” aliongeza kiongozi huyo.

Bw Odinga alisema viongozi wake hawahitaji idhini kutoka Ikulu kwenda nje ya nchi kwa sababu wako huru na wao si wafanyakazi wa serikali.

Hata hivyo, msemaji wa serikali Eric Kiraithe alipuuzilia mbali madai hayo, “Ni uongo kwa sababu ni Uganda inayofaa kuamua watu wakaoingia nchini humo,” alisema katika mahojiano.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.