Man United, PSG wavuna pakubwa katika dimba la UEFA

Taifa Leo - - FRONT PAGE -

SPOTI

KOCHA Antonio Conte amechemkia wapangaji wa ratiba ya Ligi Kuu ya Uingereza baada ya klabu yake ya Chelsea kupangiwa kuonana na Manchester City saa chache baada ya mechi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Vijana wa Conte walisakata soka safi na kuipa Atletico Madrid kichapo cha pili nyumbani katika mechi 24 za Klabu Bingwa baada ya mshambuliaji Michy Batshuayi kupachika bao lililozamisha Wahispania hao 2-1 dakika ya 93, Jumatano.

Hata hivyo, Mwitaliano huyo alilalamika kuwa City itapumzika saa 24 zaidi baada ya kulemea Shakhtar Donetsk mnamo Jumanne.

Nadhani tunaadhibiwa

“Nadhani tunaadhibiwa kidogo. Ni muhimu kutathmini hali kama hii kabla ya kupanga mechi,” alisema Conte.

“City ilikuwa nyumbani Jumanne. Sisi tumecheza mechi yetu ya Klabu Bingwa Jumatano usiku ugenini na tutarejea jijini London saa kumi asubuhi Alhamisi na tunacheza Jumamosi.”

City inaongoza Ligi Kuu kwa pointi 16 sawa na majirani Manchester United, huku Chelsea ikishikilia nafasi ya tatu pointi tatu nyuma.

“Man City ni timu kali. Wanafunga mabao mengi sana, wako katika hali nzuri wakati huu na lazima tujiandae vyema kabisa kwa mchuano huu kwa sababu una umuhimu mkubwa.

“Kabla ya kufanya uamuzi kama huu inafaa kutathmini hali ilivyo kwa makini.

“Ligi zitaenda mapumzikoni baada ya wikendi hii. Ninashangazwa na uamuzi huu kwa sababu kuna muda mwingi wa kupiga mechi hii baadaye.”

Conte aliridhishwa sana na mchezo vijana wake walionyesha walipojipata chini bao moja baada ya mvamizi Antoine Griezmann kufunga penalti dakika tano kabla ya mapumziko na kuzoa pointi zote.

Mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Alvaro Morata aliimarisha rekodi yake ya kuchana nyavu hadi mabao saba alipokamilisha krosi ya Eden Hazard kwa ustadi kupitia kichwa chake.

Morata na Cesc Fabregas kisha walimegeana pasi kabla ya Batshuayi kuzamisha Atletico kupitia kiki safi sekunde ya mwisho.

Katika mechi nyingine ya kundi hili la C, AS Roma ilizaba mabingwa wa Azerbaijan Qarabag 2-1.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.