Kamishana sasa atoa makataa kwa magenge ya wahalifu kujisalimisha

Taifa Leo - - NEWS - Na Hamisi Ngowa

KAMISHNA wa Mombasa Evans Achoki ameyapa magenge ya uhalifu katika eneo la Likoni miezi mitatu kujisalimisha.

Bw Achoki ambaye alikuwa katika mtaa wa Celtel Majengo Mapya Likoni, alisema serikali haitakubali magenge hayo kuendelea kuhangaisha wakazi. Alionya kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya vijana wanaojihusisha na mangege hayo baada ya muda huo kukamilika.

“Tumewapa nafasi vijana walio katika magenge kujitokeza na kujisalimisha kabla hatujaanza kuwasaka. Ikiwa wataendelea kushambulia na kuibia watu, ‘tutazungumza nao kwa lugha nyingine,” akaonya bila ya kutoa ufafanuzi wa matamshi hayo.

Alisema vijana hao wanafaa kuiga mfano wa wanachama wa MRC na wale wa Kaya Bombo ambao walijisalimisha kwa serikali na kwamba sasa wanaendelea na shughuli zao za kujiendeleza bila ya kuogopa serikali.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.