Kiraithe ateta siasa zinalemaza uchumi, atetea Safaricom dhidi ya madai ya NASA

Taifa Leo - - NEWS - Na Bernardine Mutanu

MSEMAJI wa Serikali Eric Kiraithe jana alisema joto la kisiasa nchini linazidi kulemaza biashara na mapato ya serikali.

Katika mkutano na wanahabari jijini Nairobi, Bw Kiraithe alisema siasa na kampeni zimeathiri mandhari ya biashara na uwekezaji nchini mbali na kuathiri nafasi za kazi.

Bw Kiraithe wakati huo huo alitetea kampuni ya mawasiliano ya simu ya Safaricom dhidi ya mashambulizi ya NASA kwa kusema madai kuwa Safaricom ilihusika katika kutatiza upeperushaji wa matokeo ya uchaguzi uliopita yalikuwa ya uongo.

Msemaji huyo alisema uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu kesi ya urais iliyowasilishwa mahakamani na Bw Raila Odinga mwezi jana haukufaa kutumiwa kushambulia Safaricom.

Hii ni kutokana na kuwa uamuzi huo ‘ulikuwa na utata’. Alisema kuwa wanasiasa wana haki ya kuchanga pesa za kufanya kampeni, lakini kuwataka kukoma kuchafulia kampuni jina au kuzitishia.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.