Huzuni na kilio mwili wa Onyancha ukiwasili kijijini

Taifa Leo - - HABARI ZA KAUNTI - Na NYABOGA KIAGE

JAMAA na marafiki wa aliyekuwa mbunge wa Bomachoge Borabu, Bw Joel Onyancha jana walifurika katika uwanja mdogo wa ndege wa Suneka kuupokea mwili wake kutoka Nairobi.

Huku wakishindwa kuzuia machozi, waliomboleza kifo cha Bw Onyancha, aliyeaga dunia wiki jana katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi.

Rais Uhuru Kenyatta, leo anatarajiwa kuhudhuria mazishi ya mwendazake ambaye amekuwa akiunga mkono serikali tangu alipojiunga na siasa.

Mwili wake ambao uliwasili saa tano asubuhi ulikuwa umeandamana na mke wake Bi Melissa Ann na familia yake.

Waliopokea mwili huo katika uwanja huo wa ndege ni pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati iliyokuwa ikishughulikia matanga yake Bw Albert Nyaundi na mwenyekiti wa Jubilee kaunti ya Kisii Bw Sam Nyairo. Mke wake wa kwanza Bi Grace Kemunto na kifungua mimba wake Denis Onyancha na majamaa wengine pia walikuweko.

Wawakilishi wa wodi ambao pia waliupokea mwili huo ni Timothy Ogugu (Kenyenya), Samwel Apoko (Kiogoro) na kiongozi wa vijana wa chama cha Jubilee Bi Esther Okenyuri.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.