Chelsea yaalika Mancity kwenye ‘gozi la mwaka’

Taifa Leo - - FRONT PAGE -

wenzangu — Nitajiunga na klabu ya majeruhi kwa mkopo kwa miezi kadhaa baada ya kuumia goti…lakini natumai nitarejea hivi karibuni na kwa nguvu zaidi,” Mendy alichapisha ujumbe kwenye mtandao wa wake wa Twitter.

Guardiola ana shinikizo kubwa kuhakikisha karibu Sh18 bilioni zilizomwagwa na City kusajili mabeki watatu zinaleta taji kubwa uwanjani Etihad. Akizungumza kabla ya hali ya jeraha la Mendy kuthibitishwa, kocha huyo Mhispania alisema, “Tuna Danilo, (Fabian) Delph na (Oleks) Zinchenko wanaoweza kucheza nafasi hiyo kwa hivyo tutaona jinsi mambo yatakavyoenda.”

City na Chelsea, ambayo iko pointi tatu nyuma ya vijana wa Guardiola na nambari mbili Manchester United, zitaingia uwanjani na motisha kubwa. Zililemea Shakhtar Donetsk na Atletico Madrid katika Klabu Bingwa Ulaya, mtawalia.

Hajafurahia ratiba hii

Lakini, kocha Antonio Conte wa Chelsea hajafurahia ratiba hii hasa kwa sababu City ilisakata mechi yake nyumbani Jumanne nayo Chelsea ilirejea nchini Uingereza mapema Alhamisi baada ya mechi yake nchini Uhispania iliyopigwa Jumatano.

“Naona ni kama tunaadhibiwa kidogo,” alisema Conte. “Kuna mapumziko ya kupisha mechi za timu za taifa baada ya wikendi hii. Sijui mbona mechi hii ililetwa mapema na kuna wakati wa kucheza baadaye,” Mwitaliano huyu aliongeza.

Washambuliaji wa Sergio Aguero, Raheem Sterling, Gabriel Jesus na Leroy Sane ni

baadhi ya miiba City inatarajiwa kutumia kuidunga Chelsea. Wanne hawa wamefunga jumla ya mabao 23 katika mashindano yote msimu huu. Hata hivyo, kuna wasiwasi kuhusu hali ya Aguero na beki Vincent Kompany. Aguero ana jeraha la mbavu naye Kompany anauguza jeraha la mguu.

Baadhi ya wachezaji wakali wa Chelsea kikosini ni Alvaro Morata, Eden Hazard, Michy Batshuayi na Victor Moses. Beki matata David Luiz hatashiriki mchuano huu. Anatumikia marufuku ya mechi tatu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu dhidi ya Arsenal mnamo Septemba 17.

City na majirani United hawajaonja kichapo ligini msimu huu. Hata hivyo, City itaanza mechi ya Chelsea kama mnyonge. Ilizabwa 3-1 uwanjani Etihad na 2-1 Stamford Bridge msimu uliopita.

United ya kocha Jose Mourinho itarukia uongozini City ikiteleza dhidi ya Chelsea nayo ilemee wavuta-mkia Palace uwanjani Old Trafford leo. United haijapoteza dhidi ya Palace katika mechi sita mfululizo. Palace pia haina ushindi wala bao katika mechi sita ligini msimu huu.

Picha/afp

Difenda wa Manchester City Benjamin Mendy akijiandaa kuingia uwanjani dhidi ya Crystal Palace awali.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.