Mazishi ya katibu mkuu ni leo

Taifa Leo - - NEWS - Na BERNARDINE MUTANU

MAZISHI ya Katibu Mkuu katika Wizara ya Ujenzi Mariamu El-maawy yaliahirishwa kutoka jana hadi leo (Jumamosi) kutokana na changamoto za uchukuzi.

Msemaji wa serikali Eric Kiraithe katika taarifa alisema kuwa mwili wa marehemu haukufikishwa nchini Alhamisi usiku kama ilivyotarajiwa kwa sababu ya changamoto za ndege.

“Changamoto zimesuluhishwa na mwili huo utawasili nchini leo, Ijumaa Septemba 29 saa nne za usiku. Mazishi yatafanyika kesho (Jumamosi) Septemba 30 saa nane mchana katika makaburi ya Kiislamu ya Lang’ata,” Bw Kiraithe alisema jana.

Bi El-maawy (pichani) aliaga dunia Jumatano katika Hospitali moja Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa baada ya kujeruhiwa na Al-shabaab katika mashambulizi ya Julai 13, Lamu.

Aliponea kifo lakini watu wengine wanne aliokuwa akiandamana nao waliuawa papo hapo akiwemo mpwawe na mlinzi wake.

Katibu huyo aliokolewa na wanajeshi waliokuwa wakishika doria na kusafirishwa hadi Nairobi kwa matibabu.

Wakati wa shambulio hilo, wanamgambo wa Al-shabaab walikuwa wakilenga kuwateka nyara katika eneo la Milihoi, katika barabara ya Mpeketoni kuelekea Lamu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.