Washukiwa wa ugaidi wanyimwa dhamana

Taifa Leo - - NEWS - Na RICHARD MUNGUTI

WASHUKIWA wawili wa ugaidi miongoni mwao mshirika wa Mohammed Ibrahim Mohammed, aliyeuawa nyumbani kwa Bw Ruto eneo la Sugoi Kaunti ya Uasin Gishu mnamo Julai 29 mwaka huu, walinyimwa dhamana na kuamriwa wazuiliwe gerezani hadi kesi zinazowakabili zisikizwe na kuamuliwa.

Akiwanyima dhamana Mabw Ali Elema Wario na Mustafa Amiana Busisa almaarufu Musty, Hakimu Mwandamizi Kennedy Cheruiyot alisema visa vya ugaidi vimesababishia nchi hii hasara kubwa ikiwa ni pamoja na shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ambapo wanafunzi 145 walipoteza maisha yao na kisa cha majuzi ambapo katibu mkuu Mariam El Maawy alishambuliwa katika Kaunti ya Lamu.

El Maawy alifariki hivi majuzi akiendelea na kupokea mataibabu nchini Afrika kusini.

“Hii mahakama inafahamu maafa yaliyosababishwa na magaidi na adhabu kali inayotolewa kwa wanaopatikana na hatia ni sababu tosha ya kuwezesha hii korti kuwanyima wawili hawa dhamana,” alisema Bw Cheruiyot.

Hakimu alikubaliana na kiongozi wa mashtaka Everlyn Maika kwamba kuachiliwa kwa washukiwa hawa wawili kwa sasa hakufai kwa vile watatoroka kukwepa kifungo kikali gerezani kisichopungua miaka 30 kila mmoja.

Wario anayetumikia kifungo cha mwezi mmoja kwa kupatikana nchini kinyume cha sheria amekana ni mwachama wa Al Shabaab.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.