Mau Mau wataka Raila awache vitisho

Taifa Leo - - NEWS - Na Joseph Wangui

KUNDI la wapiganiaji uhuru, Mau Mau, limemshauri kinara wa NASA

Raila Odinga kuachana na vitisho vya kutoshiriki uchaguzi wa marudio uliopangiwa kufanyika Oktoba 26.

Mwenyekiti wa Chama cha Wapiganiaji Uhuru Elijah Kinyua alisema kususia uchaguzi kutamfanya kupoteza nafasi katika juhudi zake za kuwa rais.

“Ikiwa Bw Odinga atakataa kushiriki uchaguzi wa marudio, Rais Uhuru Kenyatta ataapishwa moja kwa moja. Kiongozi huyo wa upinzani hafai kuogopa lakini anafaa kukabiliana na Uhuru katika uchaguzi,” alisema.

Akizungumza katika afisi za chama hicho Ruring’u, Nyeri, wakati wa mkutano na wanachama 75 kutoka kote nchini, Bw Kinyua alimshauri Bw Odinga kubatilisha maandamano yaliyopangwa dhidi ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC) na marekebisho ya sheria za uchaguzi.

Aliwashauri wanasiasa wa Jubilee na NASA kuhusika katika kampeni ya kuleta amani na utangamano kote nchini, kwa kusema siasa zimegawanya nchi.

Wapiganaji hao wakongwe zaidi walikashifu chama cha maaskofu wa Anglican ambao waliwataka maafisa wa IEBC waliokiuka sheria na kuharibu uchaguzi na kupelekea kubatilishwa kwa ushindi wa Uhuru Kenyatta kuondoka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.