Mfanyakazi wa shirika la umeme akabiliwa na kesi ya kutaka ‘kitu’

Taifa Leo - - NEWS - Na Galgalo Bocha

MFANYAKAZI wa shirika la kitaifa la usambazaji umeme Ijumaa alifikishwa mahakamani Mjini Mombasa kwa mashtaka ya kuomba na kupokea hongo ya Sh3000 ili kurudisha huduma za umeme zilizokatwa katika nyumba ya mteja wa shirika hilo.

Bw Maingi Matheka Mbatha alikabiliwa na mashtaka mawili ya kutaka hongo na moja la kupokea hongo hiyo kinyume cha sehemu ya 6 (1) na sehemu 18 (1) (2) na (3) ya sheria nambari 47 ya mwaka wa 2016 kuhusu hongo.

Katika shtaka la kwanza, Bw Maingi alidaiwa akiwa msomaji wa mita ya umeme wa shirika la Kenya Power, aliomba kupewa hongo la Sh3000 kutoka kwa Bw Abdurahman Maro kwa ajili ya kuridisha umeme katika mita yake nambari 20304650. Kosa hilo lilidaiwa kutekelezwa Septemba 20 mwaka huu katika eneo la Mishomoroni, kauntindogo ya Kisauni, Mombasa. Katika shtaka la pili, mshtakiwa alidaiwa kuomba hongo Bw Abdulrahman.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.