Gavana Sang awapa vijana vyeo vya uwaziri katika serikali yake

Taifa Leo - - NEWS - Na Philip Bwayo

GAVANA wa umri mdogo zaidi nchini Stephen Sang wa Kaunti ya Nandi ameteua vijana wanne kujumuika na watu wengine sita katika Baraza lake la Mawaziri.

Hatua hiyo ilinuiwa kutimiza ahadi yake kwa vijana wakati wa kampeni, ya kuwapa nafasi kuhudumu katika serikali ya kaunti hiyo. Gavana Sang, 33, alimteua Alfred Kiprotich, 33, kusimamia hazina ya fedha na mipango ya kifedha na Bi Valentine Chumo, 30, kusimamia utalii, utamaduni na maslahi ya kijamii.

Bw Elly Kurgat, 28, aliteuliwa kusimamia michezo na vijana hali Bw Hillary Kiprotich, 35, aliteuliwa kusimamia uchukuzi na miundo msingi. Bi Ruth Koech, 44, aliteuliwa kusimamia afya na usafi, Bw Jacob Tanui, 43, aliteuliwa kusimamia ardhi, mazingira na maliasili.

Bi Teresa Morogo, 48, aliteuliwa kama msimamizi wa shughuli katika serikali hiyo, huduma ya umma na shughuli za serikali za kielektroniki hali Dkt Bernard Kiplimo aliteuliwa kusimamia biashara, uwekezaji na viwanda.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.