Karua ataka Kuria amlipe SH2O milioni

Taifa Leo - - HABARI ZA KAUNTI - Na RICHARD MUNGUTI

KIONGOZI wa chama cha Narc-kenya Bi Martha Karua anaomba mahakama kuu iamuru Mbunge wa Gatundu Kusini Bw Moses Kuria amlipe Sh20milioni kwa kumharibia sifa kwamba waziri huyo wa zamani ndiye aliwatafuta mashahidi waliotoa ushahidi dhidi ya Naibu wa Rais William Ruto katika kesi iliyomkabili katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu(icc) mjini Hague.

Katika mawasilisho mbele ya Jaji Joseph Sergon, Bi Karua aliyewania Ugavana wa kaunti ya Kirinyaga alisema matamshi hayo ya Bw Kuria yalishusha hadhi, heshima na kumpelekea adharauliwe na wengi humu nchini. Alisema matamshi hayo ya Bw Kuria yalimkejeli na kumfanya aonekane mtu asiyestahili kutunukiwa jukumu lolote la umma.

Bi Karua aliyekuwa Waziri wa masuala ya katiba na sheria alisema kama wakili mwenye tajriba ya juu, mwanasiasa, mama na nyanya wa watoto alisema matamshi hayo ya Bw Kuria yasio na mwelekeo yalimuumiza mawazo na kumfedhehesha.

Mbunge huyo wa zamani wa Gichugu kaunti ya Kirinyaga alimweleza Jaji Sergon kwamba Bw Kuria alisema hayo Kapsokwony kaunti ya Bungoma mnamo Septemba 21 2015 wakati wa mkutano “uliodaiwa ni wa maombi ya kumwombea Bw Ruto kabla ya kuanza kusikizwa kwa kesi dhidi yake na mtangazaji Joshua arap Sang mjini Hague.”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.