Gavana mpya afuta mawaziri wote

Taifa Leo - - HABARI ZA KAUNTI - DERICK LUVEGA

GAVANA wa Vihiga Wilbur Ottichilo amewatimua kazini mawaziri wote wa kaunti waliohudumu katika serikali ya mtangulizi wake Moses Akaranga na kuwasilisha orodha mpya ya watu anaopendekeza kujaza nafasi hizo kwa bunge la kaunti hiyo ili wahojiwe.

Orodha hiyo iliwasilishwa Alhamisi jioni kuwezesha bunge la kaunti kuanza mahojiano ambayo yatachukua siku 14.

Kwa sasa, baadhi ya mawaziri katika utawala wa Bw Akaranga wanafanyiwa uchunguzi kufuatia madai kuwa walikuwa wamemezwa na tope la ufisadi.

Kwenye orodha mpya, Geoffrey Vukaya ameteuliwa kusimamia Biashara, Utalii na Viwanda huku mhadhiri wa Botswana Kenneth Keseko ameteuliwa kusimamia Uchukuzi na Miundomsingi.

Wanawake walioteuliwa ni Bi Pamela Kimwele anayepania kutwaa wizara ya Usimamizi na Mambo ya Kaunti na Bi Felistus Okumu kusimamia Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.