Korti yaipa NASA siku tano ijibu kesi

Taifa Leo - - HABARI ZA KAUNTI - JOSEPH OPENDA

MAHAKAMA Kuu ya Nakuru imeupa muungano wa NASA siku tano kujibu kesi iliyowasilishwa na walalamishi 12 wakipinga baadhi ya maafisa wa IEBC wakitimuliwa kazini.

Jaji Roselyn Korir Alhamisi alivipa vyama vya ODM, Wiper, Ford Kenya na ANC muda zaidi kuwasilisha majibu yao kabla ya kesi hiyo kusikizwa.

“Hili ni suala muhimu kwa taifa hili na vyama husika vinahitaji muda zaidi kuwasilisha majibu kabla ya kuendelea na kesi hii,” akasema jaji huyo.

Walalamishi hao ambao ni wakazi wa Nakuru, kupitia kwa wakili wao Mungai Kibe, waliwasilisha kesi hiyo kama jambo la dharura hapo Jumatano.

Pia wanataka agizo la kuzuia viongozi wa upinzani wakiongozwa na mwaniaji urais wa NASA Raila Odinga kuingilia kazi ya IEBC inayo ji taya r ishia marudio ya uchaguzi Oktoba 26.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.