Joho ataka kesi itupiliwe mbali

Taifa Leo - - HABARI ZA KAUNTI - Na Philip Muyanga

GAVANA wa Mombasa Hassan Ali Joho anataka kesi iliyowasilishwa dhidi yake na aliyekuwa seneta Hassan Omar akilenga kuchaguliwa kwake kufutwe, iondolewe.

Kupitia kwa wakili wake Paul Buti, gavana huyo alisema kutokuwepo kwa naibu wake Bw William Kingi katika kesi hiyo, kunaifanya kesi iwe wasilisho lililokosa maana.

Bw Joho anasema hatua ya Bw Omar na mgombea-mwenzake Bi Linda Shuma kukosa kumshirikisha naibu wake ni kitanzi cha kikatiba katika kesi hiyo. Gavana huyo alisema kuwa Sheria ya Uchaguzi inaelezea na kumtambua naibu gavana kama mwaniaji kwenye uchaguzi pamoja na gavana.

“Katiba, Sheria ya Uchaguzi na Mwongozo wa Uchaguzi zimetoa maelezo kamili kuhusu kuchaguliwa kwa naibu gavana moja kwa moja na wapigakura kwenye uchaguzi,” likasema wasilisho la Bw Joho. Gavana huyo anayewakilishwa pia na mawakili Dennis Mosota na Mohamed Balala aliongeza kuwa Bw Omar na Bi Shuma wamewasilisha kesi kama kitu kimoja.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.