OCS ajeruhiwa na majambazi na kuibiwa bastola

Taifa Leo - - HABARI ZA KAUNTI - Na Titus Ominde

AFISA anayesimamia Kituo cha Polisi (OCS) cha Burnt Forest, anauguza majeraha katika hospitali moja ya kibinafsi mjini Eldoret baada ya kushambuliwa na majambazi ambao walimpokonya bastola yake.

Bw Cytian Lendunda alijeruhiwa kichwani na majambazi hao alipokuwa akielekea katika nyumba yake lilioko hatua chache kutoka katika kituo hicho hapo jana usiku.

Akithibitisha kisa hicho, afisa mkuu wa polisi katika eneo la Eldoret Mashariki Bw Adamson Furaha, alisema afisa huyo anaendelea vyema na matibabu.

Bw Furaha alisema maafisa wa polisi wanaendesha msako dhidi ya majambazi husika baada ya kutoroka punde tu baada ya tukio hilo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.