Wafanyabiashara2 wakanushakuiba chakulachamsaada

Taifa Leo - - HABARI ZA KAUNTI - Na Richard Munguti

WAFANYABIASHARA wawili walishtakiwa jana kwa kuiba chakula cha msaada kilichokuwa kinapelekwa nchini Somalia chenye thamani ya Sh10million.

Mabw Abdulrahaman Hussein Abdulla na Feisal Abdikadir Abdi walikanusha mashtaka manne ya wizi wa chakula cha msaada kilichokuwa kinapelekwa nchini Somalia kutoka Nairobi.

Mshukiwa wa tatu Abdifattah

Adan Hassan hakufika kortini na Hakimu Mwandamizi Bw Kennedy Cheruiyot aliamuru atiwe nguvuni.

Pia, mahakama iliamuru dhamana ya polisi ya Sh15,000 aliyokuwa amepewa mshtakiwa ndipo afike kortini jana iliamriwa itwaliwe na Serikali.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.