Polisi watia nguvuni washukiwa sita wa ulanguzi mihadarati

Taifa Leo - - HABARI ZA KAUNTI - Na Kalume Kazungu

POLISI katika Kaunti ya Lamu wamewakamata washukiwa sita sugu wa ulanguzi wa dawa za kulevya kwenye msako mkali ulioanzishwa uliofanywa katika kisiwa cha Lamu Alhamisi jioni.

Sita hao ni Mohamed Twahir Alii, Hisham Athman Abdallah, Imran Mohamed Islam, Feiswal Mohamed Islam, Ali Hassan na Said Abdallah Mohamed.

Akithibitisha ripoti hiyo, Kamishna wa Kaunti ya Lamu, Bw Gilbert Kitiyo, alisema sita hao walikamatwa kwenye nyumba moja iliyokuwa ikishukiwa na polisi kuendeleza biashara ya dawa za kulevya mijini Lamu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.