U keketa ji kua hiri s h wa kwa dhana 2017 ina mikosi

Taifa Leo - - HABARI ZA KAUNTI - Na Vivere Nandiemo

SHUGHULI haramu za ukeketaji wasichana miongoni mwa jamii ya Kuria hazitafanyika mwaka huu kutokana dhana ya utamaduni kuwa nambari saba(mwaka 2017) ina bahati mbaya.

Haya yalidokezwa na wanajamii wa Kaunti ya Kuria na Migori na sehemu za Tanzania. Wakati kama huu kila mwaka, matabaka ya Abairege, Abanyabasi, Abagumbe na Abakira huwa yanajitayarisha kutahiri wasichana na wavulana.

Ijumaa, shirika lisilo la kiserikali, ambalo hufanya kampeni dhidi ya ukeketaji eneo hilo lilifanya kampeni katika Shule ya Msingi ya Rosabare, Kuria Magharibi.

Kupitia kwa vilabu hivyo, wanafunzi hupewa mafunzo kuhusiana na utamaduni huo uliopitwa na wakati. Zaidi ya wazee 150, viongozi na wanaharakati jana walikutana katika kituo cha Masaba kuhamasisha jamii kuhusiana na suala hilo.

“Licha ya jamii kutotekeleza shughuli ya ukeketaji mwaka huu, wanaharakati wataendelea na shughuli ya uhamasishaji,” alisema Benter Ombwayo, mratibu wa mipango katika shirika la Micontrap-kenya. Alisema wanaharakati watazidisha kampeni dhidi ya ukeketaji hasa katika vyama vya afya shuleni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.