Ashangaza waumini kukataa kuoa kanisani

Taifa Leo - - DONDOO! - Na JOHN MUSYOKI

KALAMENI mmoja kutoka sehemu hii alishangaza wengi alipobadili nia yake ya kuoa kanisani na kugeukia ndoa ya kitamaduni.

Jombi alifikia uamuzi huo wiki tatu kabla ya harusi baada ya kushawishiwa na marafiki zake kuwa huenda akapata hasara kubwa baada ya kuoa mwanadada huyo.

Inasemekana jombi alikatiza harusi na kusema ataoa demu huyo kitamaduni.

Alifika kanisani na kutangaza kuwa hatafanya harusi bali ataoa mchumba wake kitamaduni jambo ambalo lilishangaza pasta na waumini kanisani.

“Ndugu zangu, ningependa kuwaarifu kuwa harusi yangu haitafanyika kama ilivyopangwa kwa sababu nimebadili nia na kuamua kuoa mpenzi wangu kitamaduni. Niwieni radhi kwa sababu nina msukumo fulani na ndio maana nimebadili mipango yangu,” polo alisema.

Kulingana na mdokezi, tangazo hilo liliwashangaza waumini na wakataka kujua sababu ya jombi kubadili nia yake. “Kuna shida gani ya kukataa kufanya harusi na siku iko karibu kuwadia. Umepandwa na pepo ama kulikoni? Tuambie,” waumini walimuuliza jamaa.

Jombi alitoa sababu zilizomfanya kufikia uamuzi huo licha ya kutomjulisha mpenzi wake nia yake. “Hata mpenzi wangu hajui kama nimebadili nia yangu ya kufanya harusi. Nitamjulisha baadaye. Nimeafikia uamuzi huo kwa sababu zangu binafsi na sitaki presha za kufanya harusi. Tulieni hadi wakati nitakapotangaza rasmi kama kutakuwa na mabadiliko. Nimevunja kamati zote zilizokuwa zikishughulikia harusi yangu kwa sasa,” jombi alisema na badala ya kuketi kusikiliza ibada aliondoka kanisani.

Haikujulikana ikiwa atabadilisha msimamo baada ya kushauriwa na pasta na wazee wa kanisa au ikiwa mpenzi wake alikubali

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.