Mwanakwaya pabaya kujadili siasa kanisani

Taifa Leo - - DONDOO! - Na Holiness Mwambi

PASTA wa hapa alipandwa na hasira na kumfukuza mwanakwaya kwa kujadili siasa kanisani.

Duru zasema kuwa kalameni alikuwa na wanakwaya wenzake alipoanza kuzungumzia siasa na kuzua gumzo kali. Mjadala ulipamba moto na kuwafanya waanze kuongea kwa sauti za juu huku kila mmoja akitetea mrengo aliounga mkono.

Pasta aliposikia kelele alienda kuangalia kilichokuwa kikiendelea na kupigwa na butwaa kuona wanakwaya wakitaka kupigana ndani ya kanisa kwa sababu ya siasa.

Aliwazushia na kuwaagiza wakome kujadili siasa kanisani na kutimua aliyeanzisha gumzo.

“Kuanzia leo nisikuone hapa, kama wataka siasa ingia viwanjani na wanasiasa wenzako sitaki upuuzi mimi. Kanisa si mahali pa siasas, heshimu kanisa” alisema pasta kwa hasira.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.