Kibarua apoteza kazi kwa kumchapa mbwa

Taifa Leo - - DONDOO! - Na Edison Wanga

JAMAA wa hapa alifutwa kazi kwa kumpiga mbwa wa tajiri. Jombi aliyeajiriwa hapa kama dereva alikumbana na kisa hicho asubuhi mwendo wa saa mbili na nusu alipokuwa akiingia kazini.

Mbwa huyo hakuwa amefungwa vizuri ndani ya kibanda chake. Aligonga mlango na pindi ulipofunguka alitoka meno yakiwa juu juu. Jamaa alipohisi hatari, ilibidi atafute suluhu ya haraka na kuchukua kijiti akamtwanga mbwa huyo kichwani. Mbwa huyo aliruka tena kwa mara ya pili na akamwahi tena kwenye kichwa.

Baadaye jamaa alienda kwa tajiri wake kuchukua ufunguo wa gari. Badala ya kumhurumia, mdosi alimfokea. “Ufunguo wa nini? Umemjeruhi mbwa wangu halafu wataka kazi. Ondoka, Usiwahi kukanyaga hapa,” mdosi alifoka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.