Atisha kulaani mwana kujengea mama boma

Taifa Leo - - DONDOO! - Na Dennis Sinyo

MZEE wa hapa alitisha kumlaani mwanawe kwa kumjengea mama yake nyumba ya kifahari akidai kwamba hatua hiyo ililenga kutenganisha familia.

Yasemekana jamaa alipanga kutumia pesa nyingi kumjengea mama yake nyumba ya kisasa kwa kumsomesha hadi chuo kikuu baada ya baba yao kutoroka.

Baba yake alipopata habari kuhusu mipango hiyo, alimkashifu jamaa akidai alikuwa amevuka mipaka. “Ni makosa makubwa kusema utamjengea mamako nyumba na mimi sijui. Haiwezekani na ukifanya hivyo nitakula ani !’’ alifoka mzee.

Hata hivyo, jamaa alisema vitisho vya mzee vilikuwa sawa na dua la kuku ambalo haliwezi kumpata mwewe.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.