Ujumbe Mfupi

Taifa Leo - - BARUA -

MAONI: MWENYEKITI wa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi(iebc) Wafula Chebukati jana alipuuzilia mbali njama ya Jubilee kubadilisha sheria za uchaguzi akisema marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 hayahitaji sheria mpya.

Bw Chebukati alisema japo hana mamlaka ya kuingilia wajibu wa Bunge, ni vyema pande zote husika kujadiliana pamoja badala ya kuzua utata wa kubadilisha sheria za uchaguzi.je, unakubaliana naye au la? Kwa nini?

Bila shaka, nakubaliana na Bw Chebukati kuwa pande zote ambazo zinahusika zinastahili kuweka tofauti zao kado na kutafuta suluhu ya kudumu.

Samuel Plumber Muchiri, Karumandi

Nakubaliana na Bw Chebukati kwa sababu wangefanyia sheria hiyo marekebisho kitambo. Waache kwanza tufanye uchaguzi ndiyo baadaye wafanyie marekebisho sheria zao.

Charles wa Kithimu, Embu

Ingawa bunge lina mamlaka ya kutunga sheria na kubadilisha, hili halifai kwa sasa ikitiliwa maanani vile joto la kisiasa limepanda. Namuunga mkono mwenyekiti wa IEBC na nashauri Jubilee kwamba hii sheria wanapania huenda ikageuka mwiba kwao siku sijazo.

Jonah Ngari Rwigi, Kiritiri

Muda uliopo ni mchache mno kubadilisha sheria na twende kwa uchaguzi moja kwa moja.wabunge wa Jubilee waache unafiki na siasa chafu za kutumbukiza nchi hii kwa moto.

Changamka, Nakuru

Vile kuna mvutano wa vyama viwili sababu ya sheria ya uchaguzi amefanya vizuri kukataa. Jubilee walisema wako tayari kwa uchaguzi na watapita na kura nyingi kwa nini wana wasiwasi na ubinafisi. Bw Chebukati asikubali kubadilisha sheria. Sheria zilipo ni sawa kabisa. Jubilee wasicheze na wananchi kubadilisha sheria.

Kibise, Sabasaba

MJADALA WA LEO:

POLISI wamekashifiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi waliokuwa wakiandamana jijini Nairobi Alhamisi huku asasi mbili za serikali zikianzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.je, unadhani polisi wana njia bora zaidi ya kukabiliana na waandamanaji? Tupatie maoni yako

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.