Uhasama baina ya Rais Kenyatta na Odinga sumu itakayoangamiza nchi

Taifa Leo - - BARUA -

SIASA isiwe sababu ya kubomoa Kenya. Wananchi wanafaa kuwa macho wasikubali kutumiwa na wanasiasa ambao ni marafiki wakubwa licha ya tofauti zao kisiasa.

Inavunja moyo kuona viongozi wa mirengo ya Nasa na Jubilee wakiendelea kusutana hadharani. Nadhani Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wakiwa viongozi wakuu wanafaa kuelewa siasa za kusutana na kulumbana ovyovyo zinatishia uhai wa usalama sawia na uchumi nchini.

Uhasama baina ya viongozi hawa huenda ukachochea chuki za kikabila kipindi hiki cha marudio ya uchaguzi wa urais.

Amani, utulivu na upendo ndio naomba viwe dibaji kwetu wananchi walala hoi. Ni heri uishi kwa sima na sukuma kwa amani kuliko kula biriani ya kuku bila amani.

KINYUA BIN KING’ORI,

Voi

Mahakama iliamua kwa pupa

MAONI mengi yanazidi kutolewa kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Juu iliyofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanywa Agosti 8. Kwa maoni yangu, Mahakama ya Juu haikutoa uamuzi wa haki.

Hii ni kutokana na kuwa majaji walikuwa na siku 14 pekee kusikiliza kesi, kuchanganua ushahidi uliokuwa mbele yao na kutoa uamuzi.

Siku hizo bila shaka ni chache sana kusikiliza kesi kubwa kama hiyo na kutoa uamuzi wa haki. Hii ndio maana majaji hao sita waliharakisha kutoa uamuzi wao na kuwaacha wapiga kura zaidi ya millioni nane wakiwa na hasira chungu nzima. SAMUEL PLUMBER MUCHIRI, Karumandi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.